HABARI MUHIMU KUELEKEA Man utd vs CHELSEA - Darajani 1905

HABARI MUHIMU KUELEKEA Man utd vs CHELSEA

Share This

Chelsea leo itakuwa ugenini kupambana dhidi ya Manyumbu (Man utd) katika mchezo wa raundi ya 28 ya ligi kuu Uingereza ambapo mara baada ya mchezo huu wa leo itamaanisha zitakuwa zimesalia mechi 10 kumalizika kwa msimu wa 2017-2018 wa ligi kuu Uingereza.

Kuelekea kwenye mchezo huo hapa nakuletea habari muhimu zinazouhusu mchezo huo.

Habari muhimu;
Chelsea; David Luiz, Tiemoue Bakayoko na Ross Barkley ndio wataukosa mchezo wa leo kutokana na majeruhi.

Kocha Antonio Conte alipofanya mkutano na waandishi wa habari akiulizwa kama akifanikiwa kuifunga Manyumbu katika mchezo wa leo ambapo itakuwa anaifunga timu hiyo mara mbili ndani ya msimu mmoja, kocha huyo alisema itakuwa ni ujinga na ukosefu wa akili kusema kuifunga timu ndio mafanikio yako akasema kikubwa ni kutimiza kile ulichopanga kukifanya toka mwanzo wa msimu.

Man utd; Ander Herrera, Marouane Fellaini, Zlatan Ibrahimovic, Daley Blind, Marcos Rojo na Phil Jones wataendelea kukosekana kutokana na majeruhi wakati Eric Bailly anaweza kurudi kutoka kwenye majeruhi aliyokuwa nayo toka mwezi Novemba.

Mwamuzi; Martin Atkinson, ndiye mwamuzi wa mchezo wa leo huku akiwa anatajwa kuwa mmoja wa waamuzi bora kwa sasa pale Uingereza. Wakati Chelsea ilipokuwa uwanjani, ye amekuwa mwamuzi katika michezo 34 huku Chelsea ikishinda michezo 20 na kupoteza 6 huku michezo 8 ikitoka suluhu.

Rekodi; Chelsea imepoteza mchezo mmoja tu kati ya michezo 14 iliyopita katika michuano yote dhidi ya Manyumbu. Chelsea imeshinda michezo nane huku michezo mitano ikiisha kwa suluhu. Ushindi walioupata dhidi ya Chelsea ulikuwa wa 2-0 katika ligi kuu msimu uliopita.

Mechi zilizopita;
Chelsea; LLWWD
Man utd; LWLWD

Muda; Saa 05:10 Jioni (saa 17:10)

No comments:

Post a Comment