CHELSEA KUANDAA DONGE NONO KWA HAZARD - Darajani 1905

CHELSEA KUANDAA DONGE NONO KWA HAZARD

Share This
Nyota wa Chelsea, Eden Hazard amekuwa akitajwa kutakiwa na klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania ili kukiimarisha kikosi chao na kumpata mchezaji atakayeweza kuwa hatari na kuibeba timu mara baada ya nyota wake, Cristiano Ronaldo kuonekana kuanza kuachwa na soka la ushindani.

Mara baada ya kuhusishwa huko kwa muda mrefu huku kukiwa na taarifa kuwa nyota huyo mwenye miaka 27 amegoma kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea, sasa klabu hiyo imeandaa ofa nene ili kumshawishi nyota huyo asaini mkataba mpya ambapo mkataba wake wa sasa unaisha mwaka 2020.

Taarifa zinadai kuwa Chelsea imemuandalia nyota huyo fungu la mshahara la paundi milioni 15 kwa mwaka ambalo ni sawa na paundi 288,000 kwa wiki ili nyota huyo asaini mkataba mpya.

Kumekuwa na taarifa za nyita huyo kujiunga na Real Madrid ambapo uvumi huo ulivumishwa na baba yake mzee Thierry Hazard ambaye anadai nyota huyo alikataa kusaini Chelsea ili klabu ya Real Madrid imsajili ambapo baadae nyota huyo alikana na kusema ana furaha klabuni Chelsea

No comments:

Post a Comment