WILLIAN ATOA NENO KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA MAN UTD - Darajani 1905

WILLIAN ATOA NENO KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA MAN UTD

Share This
Chelsea itashuka uwanjani kesho, kupambana dhidi ya Manyumbu (Man utd) katika mchezo wa ligi kuu kwa raundi ya 28 ambapo mchezo huo licha ya kuwa mgumu, lakini pia utavuta hisia za watu wengi wakitaka kushuhudia nini kitatokea, kwanza kwa matokeo ya mchezo huo, lakini pia kwa makocha Antonio Conte kwa upande wa Chelsea pamoja na Jose Mourinho kwa upande wa Manyumbu ambapo makocha hao wamekuwa wakitupiana maneno kwa muda mrefu.

Kuelekea kwenye mchezo huo, winga hatari wa Chelsea, Willian da silva Borges ametoa neno juu ya mchezo huo utakaokuwa na watazamaji wengi wakitaka kufahamu nini kitatokea.

"Nimekuwa na kumbukumbu nzuri na Mourinho (kocha wa zamani wa Chelsea ambaye kwa sasa ni kocha wa Manyumbu), alikuwa ni kocha bora, bora zaidi kwangu, lakini sio kwangu tu hata kwa mashabiki na hata kwa Chelsea"

"Lakini kwa sasa nipo Chelsea na yeye yupo Manchester na natakiwa kuangalia upande wangu utanufaika vipi. Ni kweli sisi ni marafiki lakini linapokuja swala la uwanjani inatakiwa ufanye kazi unayopaswa kuifanya"

"Utakuwa ni mchezo mgumu, nasi kama Chelsea tunautazama mchezo huo. Ni kweli tunategemea utakuwa mchezo mgumu. Kucheza kwao sio mchezo mrahisi, tunalifahamu hilo lakini la muhimu ni kucheza katika kiwango tulichokicheza dhidi ya Barcelona" alisema nyota huyo raia wa Brazil ambaye jumanne aliiongoza vyema Chelsea kucheza dhidi ya barcelona katika mchezo wa klabu bingwa barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment