MRITHI WA COURTOIS HUYU HAPA - Darajani 1905

MRITHI WA COURTOIS HUYU HAPA

Share This
Chelsea inatajwa kwa karibu kumpoteza mlinda mlango wake namaba moja, Thibaut Courtois ambaye anahusishwa kwa karibu kuungana na klabu ya Real Madrid ambayo inatazmia kumruhusu kipa wake namba moja, Keylor Navas kondoka klabuni hapo.

Kutokana na tetesi hizo zinazovumishwa kuwa zinaweza kuwa za kweli na mwishowe nyota huyo akaondoka Chelsea, klabu hiyo imejiandaa kumtafuta mbadala mapema ili endapo kipa huyo akiondoka basi mbadala wake atakuwa ameshapatikana.

Mbadala anayetajwa kutakiwa na Chelsea ili kuja kuliziba pengo la Courtois ni kinda muitaliano ambaye kwa miaka ya karibuni amekuwa gumzo barani Ulaya haswa kutokana na umri wake na mambo makubwa anayoyaonyesha. Gigi Donnaruma, ambaye kwa sasa ana miaka 18, anatajwa kwa karibu kuja kurithi nafasi ya kipa mbelgiji, Thibaut Courtois kwenye kikosi cha Chelsea.

Mlinda mlango huyto anayepewa sifa za kuwa kipa namba moja wa timu ya taifa ya Italia, huku akifananishwa na mlinda mlango mkongwe wa klabu ya Juventus, Gigi Buffon amekuwa akitajwa kuwa mrithi wa Courtois klabuni Chelsea endapo kipa huyo akiondoka.

No comments:

Post a Comment