Katika mchezo wa jana wa ligi Kuu Uingereza ambao Chelsea ilicheza kukamilisha mchezo wake wa 19 wa ligi kuu ambao ni kama mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Uingereza imeshaumaliza, huku pia ikiweka rekodi yake ya kucheza mchezo wa 5000 kwa mashindano yote toka kuanzishwa kwake mwaka 1905, ambapo katika mchezo wa jana, huenda hii nayo ilikuwa sababu kubwa ya Chelsea kumaliza mchezo huo dhidi ya Everton kwa suluhu ya 0-0.
Kukosekana kwa mmaliziaje au namba 9 ya asili au Centre Forward (CF) huenda ilikuwa sababu kubwa ya Chelsea kushindwa kupata ushindi ambapo hilo amelikiri pia kocha Antonio Conte akisema kukosekana kwa Morata kumeiasili timu kutokana na kuwa ye ndiye mshambuliaji wa kiasili huku jana kwa nafasi yake akichez Eden Hazard ambaye kiasili sio namba 9 au sio Center Forward (CF).
Chelsea jana ilipiga mashuti 26 huku mashuti 8 yakielekea golini, lakini pia ilitengeneza krosi 30 ambazo zote hazikumpata namba 9 wa kiasili kama Alvaro Morata ambaye kiasili ni namba 9 na hata kwenye mipira ya kufunga kwa kichwa yupo vizuri.
Angeweza kucheza Michy Batshuayi ila naye bado hajawa sawa akiwa ametoka kwenye majeruhi yaliyomweka nje kwa muda kidogo.
Ingawa pia inabidi tukubali kuwa Everton jana waliingia sio kwa ajili ya kutafuta ushindi, ila kuizuia Chelsea isipate ushindi mfululizo ambapo tumekuwa tunawabaragaza misimu yote ambapo mara ya mwisho kwa Everton kupata ushindi ilikuwa msimu wa 2015-2016.
Na ukiangalia Chelsea imeshacheza michezo sita huku Eden Hazard akicheza kama mshambuliaji wa kati au namba 9, ingawa namba 9 yake yeye ikiwa ya uongo yaani "False number 9" na katika michezo yote hiyo Chelsea imepata ushindi kasoro huu wa jana dhidi ya Everton.
No comments:
Post a Comment