CHELSEA ILIPOBEBA UEFA ULIISIKIA HII? - Darajani 1905

CHELSEA ILIPOBEBA UEFA ULIISIKIA HII?

Share This

Mimi kama mwandishi na mwandaaji wa ukurasa au blog hii ya Darajani nina mapenzi makubwa na Chelsea, naamini Chelsea inaweza kufanya makubwa, sio katika mafanikio yake kama klabu ila hata kuleta karibu amani, furaha na upendo.

Na katika hilo nitazidi kukuletea mambo makubwa na ya kufurahisha ambayo labda kama uliwai kuyasikia au hukuwai kuyasikia lakini kwa uwezo alionipatia Muumba wa Mbingu na nchi nitajitahidi kukuletea kile kilicho kitamu kama mshabiki nguli wa Chelsea.

Leo nakuletea hii ambayo labda hukuwai kuiona au kuiskia.

Unaikumbuka fainali ya mwaka 2012 ya klabu bingwa Ulaya? hakuna mwana Chelsea asiyeweza kuikumbuka hii, ilikuwa ni moja ya fainali za kihistoria ndani ya Chelsea na hata duniani kiujumla.

Ndio kiduniani, kivipi nimesema kiduniani wakati kama mashabiki kikubwa tulifurahi tu kuweka historia hiyo? nasema kiduniani maana iliwakutanisha ata viongozi wakuu duniani kuuangalia mchezo huo ulioteka hisia za watu wengi duniani.

Mwaka 2012 mara baada ya kufanyika mkutano uliowakutanisha viongozi wengi wa dunia, waziri mkuu wa Uingereza kipindi iko, David Cameroon alikutana na seneta au kiongozi mkubwa wa nchi ya Ujerumani ambapo ndipo ulipokuwa unachezwa mchezo huo katika uwanja wa Allianz Arena huku timu ya taifa lake ya Bayern Munich ikicheza na Chelsea kutokea Uingereza, mama Angela Merkel walipata wahasa wa kuuangalia mchezo huo, japo hawakuuangalia wote kutokana na kuwa na mkutano ila walipata wasaha wa kuangali kile kipindi cha penati.

Lakini sio wao tu walioshiriki kuangalia matuta, ila ata rais wa Marekani wa kipindi icho, Barrack Obama nae aliangalia ingawa hakuwa shabiki mkubwa wa soka.

Penati zilipigwa huku waziri mkuu kutoka Uingereza, David Cameroon na seneta mama Angela Merkel wakiutazama na mwisho Chelsea kutoka Uingereza ikashinda ikimaanisha David Cameroon akiibuka mshindi.

Ilikuwa ni wakati mtamu sana..

David Cameroon alipohojiwa aliwai kusema "tulikuwa na mkutano, tulipata muda wa kuangalia kidogo wakati haikufikia katika penati lakini tukaenda kwenye mkutano, na baada ya mkutano kuisha tukarudi na kuangalia tena ambapo ndio tulikuta ipo kwenye penati. Obama nae aliangalia ingawa hakuwa anaelewa kuhusu mpira, ingawa nilipata tena shabiki mwengine aliyekuwa waziri mkuu wa Urusi"

No comments:

Post a Comment