CHELSEA INAMHITAJI COSTA - Darajani 1905

CHELSEA INAMHITAJI COSTA

Share This
Mara baada ya Chelsea kushinda taji la ligi kuu Uingereza msimu uliopita, mshambuliaji mwenye asili ya Brazil anayeichezea timu ya taifa ya Hispania, Diego Costa aliingia kwenye mkwaruzano na kocha wake wa Chelsea, Antonio Conte huku ikidaiwa kuwa Conte amemtumia ujumbe katika simu mshambuliaji huyo akimwambia sasa hana mipango na mshambuliaji huyo aliyeisaidia Chelsea kuvuna alama 15 katika ubingwa huo wa Uingereza. Huenda hili ndilo kosa lililofanyika, hiyo ni kutokana na mchezaji na nahodha wa Chelsea wa zamani, Denis Wise.
Denis Wise ambaye kwa sasa anafanya kazi kama mchambuzi wa soka anasema Chelsea ya sasa inamkosa mtu kama Diego Costa, inamkosa mshambuliaji ambaye anaweza kuwatisha mabeki wa timu pinzani pale ambapo Hazard, Willian na Pedro wanapokuja na mpira kushambulia.
"Alvaro Morata ni mshambuliaji wa kariba ya Harry Kane, ushambuliaji wake anafanya bila hata kuwatisha mabeki ili wafanye makosa, ila kwa Diego Costa alikuwa anawachokoza walinzi ambapo mwisho wa siku wanafanya makosa ambayo yanatumiwa vizuri na Hazard, Willian au hata Pedro" alisema Wise.

No comments:

Post a Comment