Mara baada ya mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya kwa hatua ya makundi, Chelsea ilipomenyana na AS Roma ambapo Chelsea ilipoteza mchezo huo wa kufungwa 3-0 huko jijini Roma, Italia kulitokea mzoo baina ya David Luiz na kocha Antonio Conte ambapo inaelezwa kuwa Luiz alipoambiwa kuhusu makosa aliyoyafanya katika mchezo uo hakukubali na badala yake naye akamkosoakwa mfumo aliotumia, ingawa habari hizo hazijathibitishwa. Lakini toka siku hiyo ndio ilikuwa mwisho kwa Luiz kuichezea Chelsea.
Toka baada ya mchezo huo wa ligi ya mabingwa Ulaya mpaka leo Chelsea itakaposhuka Stamford Bridge kucheza dhidi ya Brighton katika mchezo wa ligi kuu Uingereza, David Luiz atakuwa ametimiza mchezo wa 13 bila kuichezea Chelsea toka baada ya mchezo huo dhidi ya AS Roma ambapo kwa taarifa zilizokuwa zinatolewa na kocha Antonio Conte ni kuwa mchezai huyo bado ni majeruhi.
Gazeti la The Sun, liliwai kuripoti kuwa David Luiz kukaa kwake nje ni kutokana na urafiki wake na nyota wa zamani wa klabu hiyo, Diewgo Costa ambaye anasubiri dirisha la usajili la mwezi januari lifunguliwe ili ajiunge rasmi na klabu ya Atletico Madrid.
Diego Costa ambaye aliisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu Uingereza msimu uliopita aliwai akiwa mmoja wa nyota wa Antonio Conte aliondoka klabuni hapo kutokana na msuguano kati yake na kocha Antonio Conte lakini kipindi chote alikuwa na ukaribu mkubwa na David Luiz na kwa jambo hilo nadhaniwa kuwa kuwekwa nje kwa David Luiz na kocha Antonio Conte ni kutokana na mlinzi huyo kuwa karibu na Diego Costa.
Lakini pia gazeti hio linadai David Luiz kuhusika kwake kusuluhisha ugomvi uliokuwa unaendelea kati ya kocha Antonio Conte na Diego Costa ndilo linamfanya leo aadhibiwe kwa kukaa benchi huku nafasi yake kikosini ikichukuliwa na Andreas Christensen.
Kusoma zaidi taarifa hiyo bonyeza hapa>>>The Sun
DAVID LUIZ ATESWA NA DIEGO COSTA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment