Antonio Conte, kocha muitaliano aliyekuja na mafanikio makubwa klabuni Chelsea akifanikiwa kuitoa katika nafasi ya 10 ilipokuwa kabla yake mpaka kufanikiwa kuiongoza na kutwaa nayo taji la ligi kuu Uingereza katika msimu wa kwanza. Je umeshawai kuwaza nani atamrithi kama akiondoka siku moja?
Mchezaji wa zamani na gwiji wa soka aliyewai kuichezea Manchester city, Craig Bellamy amesema kama kocha huyo akiondoka siku moja basi wa kumrithi awe ni Brendan Rodgers ambaye kwa sasa ni kocha wa Celtic.
"kama ikitokea siku moja kocha Antonio Conte akiachana na Chelsea basi kocha Brendan Rodgers ndiye anatakiwa kumrithi" alisema gwiji huyo.
"ili wachezaji makinda waweze kupata nafasi katika kikosi cha kwanza basi nadhani Brendan ndiye anaweza kutimiza majkumu hayo kutokana na kuwaamini sana wachezaji makinda, na kama ingetokea siku Conte akaondoka Chelsea basi Rodgers ndiye anafaa" aliongezea Bellamy
Brendan Rodgers ambaye kwa sasa ni kocha wa klabu ya Celtic aliwai kuifundisha Chelsea akiwa katika soka la vijana akifundisha hapo kuanzia mwaka 2004 mpaka mwka 2008 kabla ya kutimkia Watford na baadae Reading na kisha Swansea kabla ya kwenda Liverpool na mpaka sasa kuwa Celtic.
MRITHI WA CONTE HUYU HAPA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment