Unamkumbuka Felipe Scolari? Ni mmoja katiya makocha ambao walikaa Chelsea kwa muda mfupi zaidi, aliingia Chelsea mwezi julai mwaka 2008 na akatimuliwa mwezi februari mwaka 2009, alidumu kwa miezi 8 tu huku sababu kubwa ya kutimuliwa kwake ikielezwa kuwa kutokana na matokeo mabovu akitoka kuiongoza Chelsea kufungwa 2-0 na Liverpool kabla ya kutoka suluhu ya 0-0 na Hull City huku Chelsea ikiwa nyumbani.
Sasa baada ya muda mrefu kupita, Scolari ameamua kuelezea sababu kubwa iliyomfanya akatimuliwa Chelsea.
"Tatizo kubwa ilikuwa kumchezesha Anelka nafasi ya winga" alieleza Felipe Scolari ambaye pia ni kati ya makocha walioowai kuzifundisha timu nyingi ambapo mpaka sasa ameshazifundisha klabu 26 akiwa kwa sasa anaifundisha klabu ya Guangzhou Evergrande.
"wakati Didier Dogba alipoumia, Nicolas Anelka alikuwa anacheza kama mshambuliaji wa kati, na alikuwa na uwezo mzuri sana akiwa mfungaji bora lakini baadae Drogba alipona na kurudi kwenye timu"
"aliporudi nilifanya nao mkutano na kumwambia Anelka inabidi ahame nafasi na kucheza kama winga, Anelka alibisha akikataa kucheza pembeni. Nami nikawaambia sipo hapa kwa ajili ya kubishana na nyinyi. Basi toka siku hiyo kukawa na mfululizo wa vituko" alielezea Scolari.
SCOLARI AJITETEA KUONDOKA KWAKE CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment