HAZARD AWA NYOTA HUKU AKIWEKA REKODI - Darajani 1905

HAZARD AWA NYOTA HUKU AKIWEKA REKODI

Share This
Nyota wa wiki hii atakuwa Eden Hazard mara baada ya kucheza soka safi jana na kuipatia Chelsea goli moja kwa kufunga kwa penati iliyosababishwa na yeye mwenyewe mara baada ya kuchezewa madhambi katika eneo la hatari la Arsenyani (Arsenal) katika mchezo ulioisha kwa sare ya 2-2.

Lakini pia katika mchezo huo, Eden Hazard aliweka rekodi mpya akiwa ndiye mchezaji aliyehusika kwenye magoli 100 yaliyofungwa na Chelsea toka ajiunge nayo mwaka 2013 akitokea klabuni Lille lakini pia ndiye akiwa mchezaji aliyeng'aa sana kwa upande wa Chelsea ambapo gazeti la The Guardian la Uingereza lilimpa alama 7/10 za kung'aa katika mchezo huo.

Nitakuwa nakujuza mengi kuhusu Hazard kwa yale ambayo huenda huyajui au unayajua kutoka kwake mpaka jumamosi ya tarehe 6-Januari ambapo Chelsea itashuka tena uwanjani kumenyana na Norwich katika mchezo wa kombe la FA.

Hongera Eden Hazard

No comments:

Post a Comment