Mara baada ya mchezo wa jana kuisha kwa suluhu ya 2-2 dhidi ya Arsenyani(Arsenal), nyota wa Chelsea mabye aling'aa katika mchezo huo, Eden Hazard ametuma lawama zake kwa kukosa ushindi huo kwamshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata mara baada ya mshambuliaji huyo raia wa Hispania kukosa nafasi tatu za wazi na kuikosesha ushindi Chelsea.
"Labda ingetakiwa tufunge magoli mengi, tulikosa nafasi nyingi" alisemaHazard. Na baada ya kuulizwa kama walistahili kushinda katika dakika za mwishoni, Hazard alijibu "Nadhani ilitakiwa liwe goli, lakini hata kabla ya hapo Alvaro alipata nafasi nyingi akakosa, nafikiri Petr Cech (kipa wa Arsenyani) alikwa kwenye ubora zaidi. Mara zote huwa ni ngumu sana kumfunga Petr" alisema Hazard
lakini pia katika mchezo uliopita dhidi ya Stoke city, Willian alilalamika kwa kusema kama Morata angekuwa bora basi angefunga magoli mawili katika mchezo huo ambao Chelsea ilishinda 5-0 huku Morata akitoka bila kufunga goli na sasa kutimiza michezo saba akicheza kama mchezaji wa Chelsea huku akifunga mara moja.
SULUHU YA CHELSEA, HAZARD AMLAUMU MORATA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment