MORATA AZUA KIZAAZAA - Darajani 1905

MORATA AZUA KIZAAZAA

Share This
huko mitandaoni ni kumewaka moto ambapo mashabiki wa soka haswa wa Chelsea wamemkurupukia mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata mara baada ya kukosa magoli matatu ya wazi katika mchezo ulioisha kwa suluhu ya 2-2 dhidi ya Arsenyani(Arsenal) ambapo mara baada ya mchezo wa jana, Alvaro Morata kupitia mtandao wa Instagram alituma picha moja wapo ya mchezo huo na kuandika maneno yasemayo "Pale mambo yanapokwenda vile usivyotarajia...pambana zaidi" ambapo ujumbe au 'post' hiyo huenda ndio ukawa ujumbe uliopata maoni mengi kutoka kwa mashabiki au watu wanaomfatilia.

Zaidi ya maoni elfu kumi (10,000) yametolewa katika ujumbe huo huku wengine wakimpa moyo na kumwambia azidi kupambana wakati wengine wakimtumia maneno makali. Nadhani huu sio wakati mwafaka wa kumlaumu maana hata mwenyewe anaonekana kuhuzunishwa na makosa hayo, na bila shaka hakupenda kuiagusha timu.

No comments:

Post a Comment