RONALDO ATAKIWA NA CONTE DARAJANI - Darajani 1905

RONALDO ATAKIWA NA CONTE DARAJANI

Share This
Chelsea inatajwa kuhusishwa kupeleka ofa ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Real Madrid raia wa Ureno, Cristiano Ronaldo ambaye anaonekana kuwa na msimu mgumu katika ligi kuu Hispania akifunga magoli manne tu msimu huu.

Chelsea ikiwa chini ya Antonio Conte inaripotiwa kupeleka ofa kwa klabu hiyo ya jijini Madrid ili imsajili nyota huyo ambaye anamiliki tunzo tano za uchezaji bora duniani huku pia kukiwa taarifa kwa klabu za PSG ya nchini Ufaransa na klabu ya LA Galaxy ya nchini Marekani inayoshiriki ligi kuu nchini humo maarufu kama MLS.

Ronaldo mwenye miaka 32 kwa sasa anatajwa kutaka kurejea nchini Uingereza huku hakuna taarifa zinazodai kwa nyota huyo kuhusishwa kutakiwa na klabu yake ya zamani ya Manyumbu (Man utd)

No comments:

Post a Comment