HAZARD KUFUNGIWA NA FA? - Darajani 1905

HAZARD KUFUNGIWA NA FA?

Share This
Jana katika mchezo wa Chelsea ilipomenyana dhidi ya Arsenal ambao uliisha kwa suluhu ya 2-2 huku Chelsea ikipata magoli yake kupitia kwa Eden Hazard na Marcos Alonso ambao goli la Eden Hazard lilipatikana kwa njia ya penati, penati ambayo ilizua utata ikionekana kama Hazard aliongopa kuangushwa na mlinzi Bellerin na kumfanya mwamuzi Taylor aruhusu kuwa ni penati.

Mara baada ya penati hiyo ambayo alipiga mwenyewe Hazard na kufunga goli hilo mzozo uliendelea na kukawa na wasiwasi kwamba huenda chama cha soka cha Uingereza maarufu kama FA kikampa adhabu nyota huyo raiawa Ubelgiji kutokana na madai hayo ya kujiangusha.

Lakini leo kumetoka taarifa kuhusu tukio hilo kwamba kumekoseakana ushahidi muhimu wa kumfanya Hazard apateadhabu kutoka kwa chama hicho na badala yake ameepuka kifungo hicho ambapo kama mngekutwa na hatia basi huenda angefungiwa michezo miwili ikihusisha dhidiya Norwich utakaochezwa jumamosi hii.

Hazard mwenyewe alipohojiwa kuhusu tukio hilo alisema "Hatuhitaji kurudia tena kuangalia ilikuwaje, ilikuwa kweli ni penati na tulistahili kushinda ingawa tumepoteza nafasi nyingi"


No comments:

Post a Comment