Mchezo wa jana wa Arsenyani ikiikaribisha Chelsea ambao uliisha kwa suluhu ya 2-2 uliweka rekodi mpya katika ligi kuu Uingereza mara baada ya kuwa mchezo wa 500 kuisha kwa suluhu kwa historia ya ligi kuu nchini humo ambapo ligi kuu hiyo ilianzishwa mwaka 1992. Ambapo kocha wa Chelsea, Antonio Conte na kocha wa Arsenyani, Arsene Wenger wakihusika katika rekodi hiyo mpya.
Arsenal dhidi ya Chelsea zenyewe zimewai kukutana uso kwa uso mara 193 toka kuanzishwa kwa klabu hizo ambapo Chelsea imeshinda mara 62 na kutoka suluhu mara 56 huku ikipoteza mara 75 wakati mchezo wa kwanza baina ya timu hizo kukutana ulichezwa tarehe 9-Novemba-1907, ambapo ilikuwa ni miaka miwili tu toka Chelsea ianzishwe mwaka 1905. Katika mchezo huo uliisha kwa Chelsea kushinda 2-1 dhidi ya washika bunduki hao ambao miaka hiyo walikuwa wakijiita Woolwich Arsenal.
Lakini pia je unajua Chelsea ilishawai kufululiza kucheza na Arsenyani katika miaka miaka 10 ikifungwa michezo miwili tu? Yaani katika miaka hiyo kumi ambapo toka mwaka 1960 mpaka mwaka 1970, Chelsea ilifungwa na Arsenyani michezo miwili kati ya michezo ishirini ambapo ilipoteza kwa 3-2 na 2-1 huku Chelsea ikishida michezo 17 na kutoa suluhu mchezo mmoja.
CONTE NA WENGER WATENGENEZA REKODI MPYA LIGI KUU
Share This
Tags
# Chelsea HD
Share This
About Darajani 1905
Chelsea HD
Labels:
Chelsea HD
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment