Kipa wa Chelsea ambaye ni rai wa Ubelgiji, Thibaut Courtois huenda akasaini mkataba mpya klabuni Chelsea muda wowote kuanzia sasa mara baada ya kuonyesha matumaini hayo akifanyiwa mahojiano mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Arsenyani.
Akihojiwa na chombo kimoja cha habari nchini Uingereza, Courtois alisema "Nina furaha ndani ya Chelsea, na huenda nikasaini hivi punde. Mimi na Eden (Hazard) ni watu ambao tunapatana sana na alisema kama utasaini basi ami nitasaini, nami nikamjibu kuwa kama yeye atasaini basi nami nitasaini" alisema Courtois akieleza kuwa hata Hazard ambaye amekuwa akitajwa kukataa kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea kuwahata yeye anakaribia kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea.
Thibaut Courtois na Eden Hazard wamekuwa wakitajwa kuhusishwa kutakiwa na klabu ya Real Madrid wote kwa ujumla, ambapo Courtois anatazamwa na Madrid ili akachukue nafasi ya kipa wa sasa, Keylor Navas ambaye anaonekana kuondoka klabuni hapo huku Eden Hazard akipendekezwa na kocha wa mabingwa hao wa ligi kuu Hispania kuwa atue klabuni hapo.
"Hata kama ukimuuza Hazard, kile kiasi utakachokipata hata ukinunua wachezaji watano, hutompata kama Hazard" alimalizia kipa huyo ambaye anatokea taifa moja na nyota huyo ambapo wote wanatokea nchini Ubelgiji.
Kwa maelezo ya Courtois inaonyesha kama Chelsea ikifanikiwa kumfanya asaini klabuni hapo basi Hazard naye atasalia ambapo hilo ndio hitaji la kila shabiki wa Chelsea. Wiki kadhaa zilizopita kurilipotiwa taarifa kuwa Chelsea ipo tayari kumpatia mkataba mpya kipa huyo utakaomfanya awe kipa anayelipwa zaidi duniani ambapo ilipangwa alipwe paundi laki mbvili (200,000) kwa wiki ingawa kukatoka taarifa kuwa Courtois amegoma kusaini mkataba huo ambao uliopo kwa sasa unaisha mwishoni mwa msimu wa 2018-2019 ikiwa ni muda sawa na mkataba wa Hazard kwa kuisha.
COURTOIS KUMSHAWISHI HAZARD ASAINI CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment