UFAFANUZI KWA CHELSEA KUPOROMOKA KLABU TAJIRI DUNIANI - Darajani 1905

UFAFANUZI KWA CHELSEA KUPOROMOKA KLABU TAJIRI DUNIANI

Share This
Najua una maswali mengi kutokana na ile takwimu na taarifa iliyochapishwa leo kuhusu klabu 100 tajiri duniani ambapo imechapishwa katika jarida la Goal.com huku Chelsea ikiwa nafasi ya 9 katika klabu hizo tajiri. Ambapo toka kufanyika kwa takwimu za msimu uliopita ambapo jarida la Total Sportek liliwai kutoa taarifa kuwa Chelsea inashika nafasi ya saba katika klabu 100 tajiri duniani lakini leo unakuja kuiona ikiwa nafasi ya tisa. Inakuwaje? kwanini iporomoke wakati msimu uliopita ilishinda taji la ligi kuu Uingereza ambalo liliipatia kiasi kikubwa cha pesa? Kwanini ipitwe na klabu kama Tottenham ambao wao wanashika nafasi ya 5 ambayo haikushinda taji lolote kubwa?

Sasa hapa nimekuletea majibu kamili kwanini umeipata takwimu hiyo ambayo huenda imekuchanganya na kukosa majibu.

Chelsea inashika nafasi hiyo ya tisa kutokana na kuwa na madeni engi yanayotokana na wachezaji waliopo kwa mkopo katika vilabu mbalimbali ambao wengi wanatokea kwenye akademi. Ipo hivi, mchezaji anapokuwa kwa mkopo akitokea klabu yoyote basi anachukua mshahara kutokea klabu aliyotokea, kwa mfano Ruben Loftus-Cheek mpaka leo anachukua mshahara kutoka Chelsea wakati kwa sasa anaichezea klabu ya Crystal Palace, Tammy Abraham ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Swabnsea kwa mkopo bado anapokea ela kutoka Chelsea iwe kwa 100% au vinginevyo vyovyote lakini kila mwisho wa wiki anapokea fungu kutoka Chelsea.

Sasa umeshajiuliza inakuwaje kwa Chelsea maana imekuwa kwenye mpango wa muda mrefu kuzalisha makinda na kuwatoa kwa mkopo kwenye vilabu vyengine au ata wengine kuuzwa kama ilivyotokea kwa Nathan Ake, Betrand Traore na Nathaniel Chalobah.

Hiyo ndio inatajwa sababu kubwa ya Chelsea kuporomoka na kufikia katika nafasi hiyo ya 9, lakini tu kama ukipigia mahesabu kwa pesa inayowalipa wale waliopo kwa mkopo ambao kwa Chelsea ni zaidi

Kwa hiyo kutokana na Forbes, Chelsea kiuhalisia ni klabu ya 7 kwa utajiri duniani ambapo utajiri wake unatajwa kufikia dola za marekani bilioni 1.85 wakati ukitoa madeni aliyokuwa nayo kutokana na kuwalipa hao waliopo kwa mkopo ndio inaporomoka mpaka nafasi ya 9. Wakati kumbe pia kiuhalisia Tottenham inashika nafasi ya 10.

Orodha hiyo ya klabu tajiri 10 ukitoa madeni (Kiuhalisia):
1. Manchester city (5)
2. Arsenal (60
3. PSG (11)
4. Guangzhou Evergrande
5. Tottenham (10)
6. Real MAdrid (2)
7. Man utd (1)
8. Juventus (9)
9. Chelsea (7)
10. Bayern Munich (4)

Vyanzo vyangu kwa taarifa zaidi ni hivi;
Total Sportek; #TS
Goal.Com; #GCOM
Forbes; #FCFC

No comments:

Post a Comment