CONTE NAYE ATAKIWA NA VIGOGO ULAYA - Darajani 1905

CONTE NAYE ATAKIWA NA VIGOGO ULAYA

Share This
Mara baada ya Chelsea kutajwa sanakatika kipindi iki cha usajili ambapo imekuwa ikihusishwa wachezaji wake kutakiwa na klabu kadhaa barani Ulaya huku kukiwa bado sintofahamu, sasa klabu hizo zimetupa ndoano kwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte.

Klabu za Bayern Munich na Paris St.Germain au PSg zinatajwa kumuwania kocha Antonio Conte mara baada ya kupendezwa na mafanikio yake katika msimu wa kwanza akiifundishwa Chelsea ambapo aliisaidia kutwaa taji la ligi kuu Uingereza huku pia ikicheza fainali ya kombe la FA.

Kocha Antonio Conte amekuwa pia akihusishwa kujiunga na klabu kadhaa nchini Italia ambapo ndipo alipotokea akija Uingereza, klabu za nchini humo za AC Milan na Inter Milan zote zinatajwa kumuwania.

No comments:

Post a Comment