Mabingwa watetezi wa ligi kuu Ujerumani, Bayern Munich inaelezwa ipo tayari kumuachia nyota wake ambaye ni kiungo mkabaji, Artulo Vidal ili aungane na Chelsea akiwa anatakiwa na kocha Antonio Conte lakini tu kama klabu hiyo itafanikiwa kumpata kiungo inayemfukuzia kutoka Schalke 04, Leon Goretzka.
Bayern ipo tayari kuachana na Vidal endapo ikimnasa kiungo huyo raia wa Ujerumani ambapo taarifa zinadai kuwa kiungo huyo anaweza akaungana na Bayern kipindi cha dirisha kubwa mwezi Juni mwaka huu ambapo mkataba wake na Schalke 04 utakuwa ukimalizika.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte inadaiwa alikuwa akifanya mazungumzo na nyota huyo raia wa Chile ambaye kocha huyo aliwai kufanya nae kazi pindi Vidal alipokuwa Juventus huku Conte akiwa kama kocha, lakini sasa anataka kuungana naye tena ingawa nyota huyo kwa sasa umri wake ni mkubwa ambapo kwa sasa ana miaka 30. Lakini pia mkataba wake klabuni huko unaisha mwaka 2019.
Je unazani Vidal ni chaguo sahihi kwa Chelsea?
BAYERN YAMLETA VIDAL DARAJANI KWA MASHARTI
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment