Mara baada ya kuwepo na taarifa kuwa Conte anaweza kuachana na Michy Batshuayi iwe kwa jumla ama kwa mkopo, kuna taarifa zikimhusu nyota wa Uingereza, Andy Carroll ambaye anaonekana kupotea katika uso wa soka kabla ya kuiokoa klabu yake ya sasa ya West Ham kunusurika kupigwa na West Brom katika mchezo wa ligi kuu juzi akifunga mara mbili.
Sasa nyota huyo naye anatajwa kuwaniwa na Chelsea ili kuweza kuchukua nafasi ya Michy Batshuayi kama mbadala wa Alvaro Morata kama akiumia au akihitajika kama mshambuliaji wa kati.
Carroll ambaye amebakiza msimu mmoja tu kwenye mkataba wake wa sasa na klabu yake ya West Ham anaweza kuondoka klabuni hapo mara baada ya kukosa nafasi kwa muda mrefu ambapo kwa sasa ana miaka 28.
Je kweli Carroll ni mtu sahihi kwa Chelsea? Unadhani atakuwa bora zaidi ya Batshuayi?

CHELSEA YATUA WEST HAM KUMSAKA MBADALA WA MICHY
Share This
Tags
# Chelsea Usajili
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Usajili
Labels:
Chelsea Usajili
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment