KINDA WA CHELSEA ATOLEWA TENA KWA MKOPO - Darajani 1905

KINDA WA CHELSEA ATOLEWA TENA KWA MKOPO

Share This
Kinda wa Chelsea mwenye asili ya Nigeria ingawa ana uraia wa Uingereza, Ike Ugbo amekamilisha usajili wake wa mkopo wa kuungana na klabu ya MK Dons ambapo atakuwa hapo mpaka mwisho wa msimu huu.

Ike Ugbo mwenye miaka 19 kulikuwa na taarifa kuwa anaweza akaunganana Chelsea kutokana na taarifa kuitwa kwake yeye pamoja na Kasey Palmer aliyekuwa akiichezea Huddersfield ambao wote walikuwa wakitajwa kuungana na Chelsea ili kuisaidia katika mzunguko.

Ike Ugbo aliyejiunga na Chelsea mwaka 2007, amejiunga na klabu hiyo akitokea Barnsley, alipohojiwa alisema "Nina furaha kuwa hapa,  katika klabu kubwa kama hii. Wachezaji wa hapa wamenifanya nijihisi vizuri na kujihisi nipo nyumbani"

Hongera kinda wetu, tunategemea uje kuwa mshambuliaji hatari baadae utakaporejea Darajani

No comments:

Post a Comment