CHELSEA YAMWINGIZA MATATANI ARSENE WENGER - Darajani 1905

CHELSEA YAMWINGIZA MATATANI ARSENE WENGER

Share This
Kocha wa klabu ya Arsenyani, Arsene Wenger huenda akapatwa na adhabu kubwa kutokana na matamshi inayodaiwa aliyoyatoa kabla na baada ya mchezo wa jana dhidi ya Chelsea. Kuna taarifa zinadai kuwa chama cha soka nchini Uingereza, FA kimemuta kocha huyo raia wa Ufaransa akidaiwa kutoa maneno mabaya dhidi wa waamuzi kabla na baada ya mchezo wa Chelsea.

Jana katika mchezo huo ambaouliisha kwa suluhu ya 2-2 huku kocha Arsene Wenger akilalamikia maamuzi ya mwamuzi wa mchezo huo Anthony Taylor kuwa hakuwa sawa katika maamuzi baina ya klabu yake ilipomenyana jana katika uwanja wa Emirates.

Kupitia taarifa kutoka FA inasema "Chama cha FA kimeamua kufanya uchunguzi kutokana na maneno aliyoyaongea Arsene Wenger kupitia vyombo vya habari siku tarehe 02-Januari na baada ya mchezo dhidi ya Chelsea. Mwisho wa kuripoti iwe tarehe 09-Januari saa 12:00 jioni"

Huenda kocha huyo akakutwa na adhabu kali kutoka kwa chama hicho mara baada ya kuwa matatani pia kutoakana na kubishana na mwamuzi Mike Dean katikamchezo wa ligi kuu uliopita dhidi ya West Brom na katika mchezoo wa jana alikuw kwenye adhabu akiwa alikatazwa asiuguse mstari wa eneo la uwanja.

No comments:

Post a Comment