BARKLEY HUYU HAPA DARAJANI - Darajani 1905

BARKLEY HUYU HAPA DARAJANI

Share This

Usajili wa Ross Barkley kutua Chelsea unatajwa kufikia hatua za mwisho kukamilika mara baada ya kuwepo taarifa za kuthibitisha kuwa winga huyo machachari kutokea Everton ametua jijini London ili kumalizana na mabingwa hao watetezi.

Ross Barkley anatajwa kujiunga na Chelsea kwa dau la paundi milioni 15 kutokea klabuni hapo ambapo inaelezwa kocha wake wa Everton anatajwa kuthibitisha taarifa hizo.

Kama una kumbukumbu vizuri, Barkley alikuwa katika mipango ya kocha Antonio Conte tangu mwezi Agosti mwaka jana katika dirisha kubwa la usajili na ilibaki kidogo atue Chelsea kabla ya nyota huyo kughaili na kusema atarudi tena endapo akishapona kabisa majeruhi yake. Na sasa anaelezwa kuwa vizuri mara baada ya kuwai kuripotiwa kuwa amerejea mazoezini.

Karibu Darajani Barkley.

No comments:

Post a Comment