ALIYEKUWA NYOTA WA CHELSEA ASHINDA TUNZO AFRIKA - Darajani 1905

ALIYEKUWA NYOTA WA CHELSEA ASHINDA TUNZO AFRIKA

Share This

Aliyewai kuwa mchezaji nyota wa Chelsea, Mohammed Salah amechaguliwa rasmi kuwa mchezaji bora wa Afrika na chama cha soka barani humo maarufu kama CAF.

Salah ameshinda tunzo hiyo ambapo ameiongoza vyema timu yake ya taifa ya Misri kuweza kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 huku pia timu hiyo ikichaguliwa kuwa timu bora ya mwaka 2017.

Salah aliwai kuichezea Chelsea mwaka 2013 akitokea Fc Basel ambapo hakucheza Chelsea kwa mafanikio makubwa akitumia muda mwingi kuingia kama mchezaji wa akiba na hivyo kutolewa kwa mkopo klabuni Fiorentina na baadae As Roma nchini Italia kabla ya klabu hiyo kuamua kumsajili moja kwa moja. Na msimu uliopita akajiunga rasmi na klabu ya Liverpumba ya nchini Uingereza.

Salah ameshinda tunzo hiyo huku Sadio Mane akishika nafasi ya pili na ya tatu kuchukuliwa na Pierre Aubameyang.

Lakini kulikuwa na mzozo mkubwa kutoka kwa baadhi ya raia na wapenda soka wakihoji mafanikio aliyoyapata nyota huyo kwa ngazi ya klabu kutokana na kutoisaidia As Roma (aliyokuwa akiichezea kwa mwaka 2017 kabla ya kuamia Liverpumba) kutokana na kutoisaidia kushinda taji lolote huku Victor Moses wa Chelsea ambaye ni raia wa Nigeria ambaye aliisaidia Chelsea kutwaa taji la ligi kuu Uingereza lakini kuisaidia timu ya taifa kufuzu kucheza kombe la dunia.

Je unazani ni tunzo sahihi kwa Salah au kulifanyika  uonevu?

No comments:

Post a Comment