Kuna taarifa zinaripotiwa na mwandishi Matt Law kuwa kiungo na winga wa klabu ya Everton, Ross Barkley amebakiza kufanyiwa vipimo na klabu ya Chelsea ili asaini na kuwa mchezaji rasmi wa Chelsea.
Ross Barkley inaelezwa kuwa tayari yupo jijini London ili kukamilisha taratibu hizo za usajili ambapo mara baada ya vipimo vinavyoelezwa kufanyika hii leo huenda akatangazwa rasmi kuwa mchezaji mpya wa Chelsea kwa dau la paundi milioni 15.
Barkley ilikuwa atue Chelsea toka dirisha kubwa la usajili la mwezi Agosti mwaka jana kabla ya kuhairisha kumalizia taratibu hizo kutokana na kuwa majeruhi.
No comments:
Post a Comment