Kocha wa klabu ya Atletico Madrid, Diego Simeone amependekezwa na ata kuonekana ndiye atakuja kuwa mrithi au wakuvaa viatu vya kocha wa sasa wa Chelsea, Antonio Conte.
Katika gazeti la Times la nchini Uingereza limechapisha habari kuhusu nafasi ya kocha huyo kutua klabuni Chelsea endapo kocha wa sasa, Antonio Conte ataachana na klabu hiyo.
Conte amekuwa akitajwa kwa muda mrefu kutaka kuondoka klabuni hapo kutokana na kutokuwa na mahusiano mazuri kati yake na bodi ya timu hiyo ambapo mara kadhaa kocha huyo amekuwa akikana tuhuma hizo.
Lakini sasa kuachana na klabu hiyo kunaonekana kuchochea mara baada ya kuhusishwa kutakiwa na klabu za Bayern Munich, PSG na klabu za jiji la Milan yaani AC Milan na Inter Milan.
Lakini pia taarifa zinaeleza kuwa Diego Simeone mwenyewe anataka kwenda kufundisha nchini Italia ambako huko anakiongea vizuri lugha ya kiitaliano kuliko kiingereza.
Makocha wengine wanaotwaja kuwaniwa ni Maxi Allegri na Maurizio Serri.
No comments:
Post a Comment