Huenda mchezo wa juzi kati ya Chelsea dhidi ya Arsenyani uliochezwa pale uwanja wa Emirates ukiisha kwa suluhu ya 2-2 ukaendelea kuzusha mengi mara baada ya leo tena kutoka taarifa kuwa kocha wa Arsenyani anataka kufanyiwa vipimo vya akili kutokana na maneno aliyoyaongea baada ya mchezo huo.
Kocha huyo alipohojiwa baada ya mchezo huo aliongelea shuti kali lilopigwa na Zappacosta dakika za majeruhi za mchezo kuwa kama lingeingia goli basi angejiua. Ilieleweka kuongea kwake hivyo alitania lakini mtaalamu mmoja wa nchini Uingereza, Allison Kerry amesema hiyo ni kauli mbaya kwa kuongewa na mtu yoyote aliye timamu maana inaleta wasiwasi kuwa huenda akili yake ina matatizo na huenda akajiua kwa kile chanzo kinachojulikana kama upungufu wa afya ya akili.
Yaani ipo hivi, kusema kwake huko huenda kama kweli Zappacosta angefunga lile goli ambalo liligonga mwamba basi mshtuko wa kocha huyo ungemfanya ajiue kweli bila kudhania.
"Kumekuwa na matukio mengi ya mtu kujiua mwenyewe, ambapo katika vifo 5000 vilivyolipotiwa katika nchi za Uingereza na Wales kwa mwaka 2016 ilielezwa sababu mojawapo ni afya ya akili ambayo mwishowe mtu anajiua mwenyewe. Kila siku kunaripotiwa vifo vya watu 13 huku ikiwa sawa na watu wawili kujiua kwa kila masaa mawili, kwa hiyo haikupaswa kwa Wenger kutamka maneno kama yale. Huenda angefanya kweli" alisema mtaalamu huyo.
Lakini pia Wenger anafanyiwa uchunguzi na chama cha soka nchini Uingereza maarufu kama FA kutokana na kauli zake alizozitoa kabla na baada ya mchezo wa Chelsea hapo juzi.

WENGER KUCHUNGUZWA AKILI KISA CHELSEA
Share This
Tags
# Majirani
Share This
About Darajani 1905
Majirani
Labels:
Majirani
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment