CONTE KUPAMBANA TENA NA GUARDIOLA - Darajani 1905

CONTE KUPAMBANA TENA NA GUARDIOLA

Share This
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte ameingia katika mpambano mkali na kocha Pep Guardiola wa Mama site ambapo safari hii wanagombania tunzo ya kocha bora wa mwezi Desemba ambapo mpambano huo unawahusisha makocha sita huku wanaoonekana kuchuana kwa karibu ni Antonio Conte na Pep Guardiola.

Kocha Antonio Conte katika mwezi huo wa Desemba ameiongoza Chelsea kushinda michezo 5 na kusuluhu mmoja huku akipoteza mmoja dhidi ya West Ham wakati Pep Guardiola akiwa ameshinda michezo 5 na kusuluhu mmoja huku hakuna aliopoteza.

Makocha wengine wanaogombania tunzo hiyo ni Sam Allardayce wa Everton ambaye kati ya michezo saba ameshinda 3 suluhu 3 na kufungwa mmoja, Roy Hodgson ameshinda 2 amesuluhu 4 na kufungwa mmoja, Jurgen Klopp wa Liverpunga akiwa ameshinda 4 na kusuluhu 3 huku hakuna aliopoteza na Mauricio Pochettino wa Tottenham ambaye ameshinda 4 akisuluhu mmoja na kufngwa mmoja.

Je unazani kuna nafasi kwa Conte kushinda tunzo hiyo?

No comments:

Post a Comment