Mara baada ya kocha wa Chelsea, Antonio Conte kutoa ruhusa kwa mchezaji yoyote kama anahitaji kuachana na klabu hiyo ya Chelsea kwa kuhofia kukosa nafasi katika timu zao za taifa kuelekea kombe la dunia mwaka huu litakaloanza mwezi Juni, mlinzi wa klabu hiyo ambaye ni raia wa Brazil, David Luiz inaelezwa amemwambia wakala wake amtafutie klabu nyengine mpa mara baada ya kuona nafasi yake klabuni Chelsea ni ngumu.
David Luiz aliichezea Chelsea mchezo wake wa mwisho toka mwezi Oktoba katika mchezo ambao Chelsea ilipoteza 3-0 kwa klabu ya As Roma katika michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya ambapo toka baada ya mchezo huo Andreas Christensen amekuwa akipata nafasi kama mbadala wa nyota huyo.
Sasa taarifa ndio zimetoka kuwa mchezaji huyo amemweleza wakala wake kuwa amtafutie klabu nyengine lakini inaonekana dili lake kutua klabuni Barcelona ni ngumu kutokana na klabu hiyo kuonekana inawaamini walinzi wake Gerrard Pique na Samuel Umtiti ambapo pia kama Luiz akijiunga na klabu hiyo hatoruhusiwa kucheza mchezo wowote wa ligi ya mabingwa msimu huu kutokana na kuhusika tayari akiwa klabuni Chelsea.
Ni nini hatma ya David Luiz? Hakuna anayejua ingawa kocha Antonio Conte alisema huenda akarejea uwanjani jumamosi (kesho) katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Norwich.

LUIZ BADO HAKIJAELEWEKA CHELSEA
Share This
Tags
# Chelsea Habari
Share This
About Darajani 1905
Chelsea Habari
Labels:
Chelsea Habari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment