JUVENTUS YAKERWA NA BARKLEY KUTUA CHELSEA - Darajani 1905

JUVENTUS YAKERWA NA BARKLEY KUTUA CHELSEA

Share This
Kwa taarifa zilizopo zinadai kuwa nyota raia wa Uingereza wa klabu ya Everton, Ross Barkley ni kama tayari ahatua Chelsea mara baada ya kuwepo taarifa kuwa nyota huyo anafanyiwa vipimo leo ili atue klabuni Chelsea. Lakini je wajua kuwadili hilo ni kama nuksi kwa klabu ya Juventus?

Ndio ni kama nuksi kwa mabingwa watetezi hao wa ligi kuu Italia maarufu kama Serie A mara baada ya kuwepo taarifa kuwa kumbe Chelsea na Juventus zilikuwa zinafanya mawasiliano ya chini kwa chini ili kiungo wa mabingwa watetezi hao, Claudio Marchisio aungane na Chelsea.

Inaelezwa kuwa kocha Antonio Conte alikuwa na mpango wa kumsajili kiungo huyo ambaye aliwai kufanya nae kazi akiwa klabuni Juventus na timu ya taifa ya Italia ambako kote huko alikuwa kama kocha na Marchisio kama mchezaji, na ilikuwa waungane tena klabuni Chelsea ambapo mpango huo ulishafikia mahali p[azuri, lakini sasa biashara hiyo inaonekana kufa mara baada ya Chelsea kumpata Barkley.

Lakini pia inaelezwa Conte alikuwa anamhitaji kiungo ambaye kwanza ni mdogo kiumri kwa kuwa Cesc Fabregas anaelekea kutimiza miaka 31 huku Pedro na Willian wanatimiza miaka 30 mwaka huu lakini kwa Barkley ana miaka 24 huku Marchisio ana umri wa miaka 31 lakini pia alimhitaji kiungo raia wa Uingereza kutokana na sheria za ligi kuu Uingereza kutoruhusu timu kucheza bila raia wa Uingereza.

Kwa maana hiyo sasa ni kama Juventus inabidi itafute klabu nyengine ya kumuuza kiungo huyo ambaye mkataba wake na Juventus unaisha mwaka 2022.

No comments:

Post a Comment