MARCOS ALONSO MCHEZAJI BORA UINGEREZA? - Darajani 1905

MARCOS ALONSO MCHEZAJI BORA UINGEREZA?

Share This
Mara baada ya kocha Antonio Conte kuingia kwenye mchuano wa kutafutwa kwa kocha bora wa mwezi Desemba ambapo akigombea tunzo hiyo ya ligi kuu Uingereza na makocha kama Guardiola na Jurgen Klopp, sasa tena nyota wa Chelsea, Marcos Alonso naye amechaguliwa kugomea tunzo ya mchezaji bora wa mwezi huo wa Desemba mwaka jana.

Marcos Alonso ambaye juzi alitoka kuweka rekodi ya kuwa mlinzi au beki mwenye magoli mengi katika ligi tano bora za Ulaya akiwa na magoli 6, ameingia kwenye mchuano wa kugombania tunzo hiyo akiwa pamoja na Mohammed Salah (Liverpumba), Harry Kane (Tottenham), Jesse Lingard (Manyumbu), Roberto Firmino (Liverpumba), Nicolas Otamendi (Mama site), Riyad Mahrez (Leicester) na Marko Arnautovic (West Ham).

Je unazani Marcos Alonso ana nafasi ya kushinda tunzo hiyo?

No comments:

Post a Comment