BARKLEY AFUZU VIPIMO, TAYARI KUJIUNGA CHELSEA - Darajani 1905

BARKLEY AFUZU VIPIMO, TAYARI KUJIUNGA CHELSEA

Share This

Taarifa zinazoripotiwa na Skysports ni kuwa winga na kiungo Ross Barkley tayari ameshafanyiwa vipimo na kuonekana amefuzu.

Kiungo huyo raia wa Uingereza alichokibakiza kwa sasa klabuni Chelsea, ni kusaini tu mkataba ambapo yeye pamoja na wawakilishi au wakala wake tayari wapo Stamford Bridge ili kumaliza taratibu zote za nyota huyo mwenye miaka 24 kutua rasmi Chelsea.

Usajili unatajwa kuigharimu Chelsea kiasi cha paundi milioni 35 ambapo mchezaji huyo amebakiza miezi sita tu kwenye mkataba aliokuwa nao na klabu ya Everton.

Chelsea itatangaza rasmi kusainiwa kwa mchezaji huyo muda mfupi kuanzia sasa.

No comments:

Post a Comment