Mlinzi wa Chelsea, kinda Andreas Christensen amechaguliwa rasmi kuwa mchezaji bora mwenye kipaji adhimu uko nchini kwao Denmark.
Andreas amekuwa na kiwango bora tangu ajiunge na Chelsea na kupelekwa kwa mkopo katika timu ya ligi kuu Ujerumani maarufu kama Bundesliga ambako huko alishinda tunzo ya mchezaji bora wa klabu hiyo ya Borrusia Monchnglebach katika msimu wake wa kwanza wa mkopo klabuni hapo. Kisha msimu huohuo wa 2015-2016 akachaguliwa pia kuwa mchezaji bora mwenye kipaji bora nchini kwake Denmark.
Christensen amekuwa akiaminiwa na kocha Antonio Conte huku akionekana kuwa mbadala wa mlinzi David Luiz ambaye amekuwa akitumika zaidi toka kupoteza kwa Chelsea mbele ya As Roma ambao ndio ulikuwa mchezo wa mwisho kwa Luiz kuichezea Chelsea msimu huu.
Hongera kwako Andreas Christensen.
No comments:
Post a Comment