ALICHOKISEMA CONTE KUELEKEA NORWICH vs CHELSEA - Darajani 1905

ALICHOKISEMA CONTE KUELEKEA NORWICH vs CHELSEA

Share This
Kama ilivyo kawaida ya kocha Antonio Conte kufanya mkutano na waandishi wa habari siku moja kabla kuelekea mchezo ambao Chelsea itashuka uwanjani, basi leo tena kocha huyo muitaliano amefanya mkutano mwengine kuelekea kesho ambapo Chelsea itacheza mchezo wake wa kombe la FA dhidi ya Norwich, hichi ndicho alichokizungumza;

Kuhusu Ross Barkley
Kocha Antonio Conte alijibu "Mtapata habari zaidi kutoka kwa klabu, ila ni habari nzuri na jambo jema pia kweu kama klabu. Ni raia wa Uingereza na ana umri mdogo bado. Anamuda mrefu wa kuonyesha kiwango na ubora wake. Nadhani jambo muhimu kwa sasa ni kujua lini atapona na kurejea uwanjani haraka maana alipata majeruhi makubwa na yalimweka nje kwa muda mrefu. Amekaa bila kucheza kwa miezi saba muhimu ni kutumaini kama atapona mapema na kuungana na klabu"


Kuhusu Andy Carroll
Conte alijibu "sijui, niliipatia klabu maoni yangu kuwa ni nani namuhitaji ila wao ndio wakuamua ni nani wa kuuzwa na nani wa kununuliwa"


Kuhusu nafasi yake kuchukuliwa na Simeone
Conte alijibu "Nadhani tunazipata habari nyingi, haswa kipindi iki haswa kunihusu mimi. Kama mnavyotambua kuwa mahali hapa ni historia kubwa. ni kawaida kwa kocha muhimu kupata habari na fununu kama hizo"


Kuhusu Wenger aliposema kuwa Hazard alijiangusha
Conte alijibu "Nadhani kama Arsene(Wenger) akirudia kuuangalia ule mchezo kwa mara nyingine basi atatambua kuwa alikuwa na bahati sana na maamuzi ya mwamuzi"


Kuhusu Mourinho kumuongelea (Conte) kuhusu ushangiliaji wake
Conte alijibu "Nadhani alikuwa najiongelea mwenyewe aliyokuwa anayafanya hapo kabla, muda mwengine mtu unasahau uliyowai kuyafanya"












Kuhusu aina ya soka anayocheza Morata, na je ameweza kuziba pengo la Diego Costa?
Conte alijibu "Mpaka sasa takwimu zake zinasema kuwa amefunga magoli 12 na kutengeneza mengine 7, nadhani ni takwimu nzuri kwake kutokana kwanza ni mdogo, ana miaka 25 tu, mimi pamoja na klabu tuna furaha kwa mafanikio aliyafikia mpaka sasa ukilinganisha ana muda mfupi kwenye ligi"
 
Kuhusu makocha wa klabu nyengine wanaomuongelea (Conte)
Conte alijibu "Huwa sipendi kuzungumzia wachezaji au makocha wengine, lakini nashangazwa na makocha wengine hawana hiyo tabia. Ni njia rahisi ya kumuonyesha mtu kwa kiasi gani unamheshimu ila namshangaa Wenger anapenda kuzungumza kuhusu sisi, na labda akumbukwe tu, katika michezo kadhaa ambayo tumecheza dhidi yake tulimaliza tukiwa wachezaji 10 tu"
 
Kuhusu Wilshere kutopewa kadi nyekundu katika mchezo wa Arsenal vs Chelsea, juzi
Conte alijibu "Nilikuwa na uwezo wa kulalamikia jambo hilo karibu hata mwenzioi mzima, ila siwezi japo maamuzi ya mwamuzi hayakuwa sahihi. Inabidi tukubaliane na maamuzi ya mwamuzi. Ata Wenger naye inabidi akubali"
Kuhusu kubadili kikosi katika mchezo dhidi ya Norwich, kesho
Conte alijibu "Nina imani na wachezaji wangu, David Luiz atakuwa tayari katika mchezo huo lakini tatizo lililopo kwa sasa ni Eden Hazard kutokana na kupata majeraha dhidi ya Arsenal. Inabidi tujaribu kuona tutalimalizaje hilo tatizo.

No comments:

Post a Comment