CHELSEA NA YOKOHAMA KWENYE KUMBUKUMBU - Darajani 1905

CHELSEA NA YOKOHAMA KWENYE KUMBUKUMBU

Share This
Siku kama ya leo, mwaka 2015, Chelsea ilifanikiwa kukamilisha dili la kusaini udhamini na kampuni ya matairi ya Yokohama, dili lililokuwa na thamani ya paundi milioni 40 kwa mwaka ambapo mkataba huo ni wa miaka mitano, ambapo pia kwa usajili wa udhamini huo, uliifanya Chelsea kuwa klabu ya pili kuwa na uddhamini ghali kwenye ligi kuu nchini Uingereza kwa upande wa matangazo ya jezi.

Kwa dili hilo, Chelsea ilizipiga vikumbo klabu kama Arsenyani (Arsenal), Mama site (Man city) pamoja na Liverpumba (Liverpool) huku ikiachwa na Manyumbu (Man utd) ambao ndio wanapokea dau kubwa kuzidi Chelsea, wanapokea paundi milioni 53 kwa mwaka kutoka kwa Chevrolet.

No comments:

Post a Comment