CHELSEA KUMUWANIA NYOTA KUTOKA IVORY COAST - Darajani 1905

CHELSEA KUMUWANIA NYOTA KUTOKA IVORY COAST

Share This
Chelsea inatajwa kumfukuzia nyota raia wa Ivory Coast, Yann Karamoh ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo klabu ya Inter Milan ya nchini Italia huku klabu yake ikiwa ni klabu ya nchini Ufaransam, klabu ya Can ambayo imemtoa kwa mkopo wenye kipengele cha kusajiliwa kabisa na Inter Milan endapo wataridhika na kiwango chake.

Lakini nyota huyo natajwa kuvutiwa haswa na mpango wa kutakiwa na klabu ya Chelsea ambayo ilipeleka waangalizi ili kumwangalia akiwa uwanjani akisakata kabumbu. Nyota huyo ana miaka 19 kwa sasa, huku akitajwa kuwa na kipaji cha hali ya juu mpaka kuvivutia vilabu vikubwa barani Ulaya huku Chelsea ikitajwa kuwa klabu mojawapo, ikiwa sambamba na Barcelona ambao nao wanatajwa kumuwania.

No comments:

Post a Comment