NYOTA WA CHELSEA KUTIMKIA MAREKANI - Darajani 1905

NYOTA WA CHELSEA KUTIMKIA MAREKANI

Share This
Nyota wa Chelsea Ladies ambayo nim klabu kwa ajili ya wanawake, Crystal Dunn anakaribia kuondoka kwenye klabu hiyo na kujiunga na klabu ya North Carolina Courage ambao wametajwa kukamilisha usajili wa kumng'oa nyota huyo anayecheza nafasi za winga-beki au winga.

Nyota huyo mwenye miaka 25 alijiunga na Chelsea Ladies mwaka mmoja uliopita akitokea klabu ya Washington Spirit ambapo mara baada ya kufika Chelsea, akawa anatumika zaidi kama mshambuliaji wa kati kabla ya baadae kuamishwa na kuanza kutumika kama winga katika kikosi cha kocha mwanamama, Emma Hayes ambaye ameingia kwenye kinyang'anyiro cha kugombania tunzo kama kocha bora wa mwaka 2018 katika tunzo za London.

Dunn ameisaidia Chelsea kushinda mataji ndani ya muda huo mfupi akiisaidia vyema pia kushiiriki ligi ya mabingwa Ulaya kwa wanawake na kufikia hatua ya robo fainali kwa mara ya kwanza.

Nyota huyo alipohojiwa juu ya kuondoka kwake klabuni Chelsea, alisema "Ni ngumu kuondoka klabuni hapa, lakini inanibidi nifanyew hivi kutokana na mahitaji ya soka langu na mambo yanayoknikabiri, kurudi kwangu Marekani ni maamuzi mazito kuyafanya"

"nashukuru kila jambo lililotokea klabuni hapa, na kwa jinsi walivyonielewa na kuelewa nini kuhusu mimi, nitakuwa na kumbukumbu nzuri kuhusu klabu hii. Napenda kumshukuru Emma (kocha wa Chelsea ladies) kwa kuwa karibu nami na benchi lake la ufundi, lakini pia kwa wachezaji wenzangu kwa sio tu kuwa bora, ila pia kwa kuwa marafiki kwangu, lakini pia kwa mashabiki wote wa Chelsea waliokuwa pamoja nami"

"Ni muda mzuri nimetumia kuwa hapa, na hakika ndani ya moyo wangu kutaendelea kuwepo upendo wangu kwa Chelsea FC" alisema nyota huyo raia wa Marekani.

No comments:

Post a Comment