BATSHUAYI KUIPELEKA KLABU YA ITALIA MAHAKAMANI - Darajani 1905

BATSHUAYI KUIPELEKA KLABU YA ITALIA MAHAKAMANI

Share This
Chama cha soka barani Ulaya maarufu kama Uefa, kinaweza kikaidhibu klabu ya nchini Italia, Atalanta mara baada ya kuwepo tuhuma zilizoibuka juu ya mchezo wake ilipomenyana dhidi ya klabu ya Borrusia Dortmund katika michuano ya Europa League maarufu kama Uefa Ndogo ambapo walimzomea mchezaji wa Chelsea anayecheza kwa mkopo kwenye klabu ya Borrusia Dortmund, Michy Batshuayi.

Ilikuwa katika mchezo wa marudiano wa michuano hiyo ambapo Dortmund ilikuwa ugenini kucheza mchezo wake wa pili wa hatua ya 32 bora ya michuano hiyo nchini Italia kwenye uwanja wa Atalanta ambapo mchezo wa kwanza Dortmund ilishinda ikiwa nyumbani kwa mabao 3-2. Na katika mchezo huo wa marudiano, mchezo huo uliisha kwa suluhu ya 1-1 ambapo kwa matokeo hayo yalimaanisha Dortmund ilifanikiwa kufudhu kwa magoli ya jumla ya 4-3, ndipo mara baada ya mchezo nyota huyo wa Chelsea raia wa Ubelgiji alieleza kusikitishwa kwake na ubaguzi wa rangi alioonyeshwa na mashabiki wa timu pinzani wakipiga kelele za nyani kumaanisha mchezaji huyo ni kama nyani kutokana na rangi yake.

Na sasa chama cha soka barani humo ambacho kimekuwa kikipinga ubaguzi wa rangi kimepanga kulivalia njuga swala hilo, kimepanga kufanya kufanyia uchunguzi na kutoa hukumu kwa klabu ya Atalanta ambayo imekuwa na mfululizo wa matukio ya ubaguzi ambapo kesi hiyo imepangwa kufanyika tarehe 22-Marchi mwaka huu.

Nilikuletea habari hiyo kuhusu tukio hilo, ili kuisoma zaidi, bonyeza hapa

No comments:

Post a Comment