CHELSEA KUMVUTA NYOTA WA KIBRAZIL KUTOKA AS ROMA - Darajani 1905

CHELSEA KUMVUTA NYOTA WA KIBRAZIL KUTOKA AS ROMA

Share This
Chelsea ina mpango wa kumsajili nyota mwengine kutoka klabu ya As Roma. mara baada ya kuwasajili nyota wawili kutoka klabuni hapo ambao ni Antonio Rudiger pamoja na Emerson Palmieri sasa Chelsea inatajwa kumtaka nyota mwengine wa klabu hiyo ambaye ni mlinda mlango.

Chelsea inatajwa kumtaka mlinda mlango wa klabu hiyo, Allison Becker ambaye ni mlinda mlango namba moja wa timu ya taifa ya Brazil. Lakini Chelsea itaingia kwenye vita ya kumsajili mbrazili huyo kama tu mlinda mlango wa sasa, Thibaut Courtois ataendelea na mpango wake wa kutotaka kusaini mkataba mpya klabuni Chelsea.

Katika kuitafuta habari hii ya kipa huyu kutakiwa na Chelsea endapo Courtois atasaini mkataba mpya, Darajani 1905 imekutana na maoni ya mshabiki mmoja ambaye alitoa maoni yake juu ya taarifa hizi akisema "Tafadhali (Thibaut Courtois) mwacheni aondoke tu. Caballero bado anaweza kudaka kwa miaka miwili. Hivi Petr Cech angejiuliza mara mbili kama angeambiwa asaini mkataba mpya pindi alipokuwa Chelsea?"

Je una maoni gani katika hili:?

No comments:

Post a Comment