CONTE AELEZA SABABU YA KUMTOA HAZARD - Darajani 1905

CONTE AELEZA SABABU YA KUMTOA HAZARD

Share This
Chelsea imeporomoka kutoka kwenye nafasi nne za juu katika msimamo wa ligi kuu Uingereza mara baada ya kupoteza mchezo wake wa jana dhidi ya Manyumbu (Man utd) kwa magoli 2-1. Katika mchezo huo, dakika ya 73 wakati mchezo ulipokuwa na matokeo sawa ya 1-1, kocha Antonio Conte aliamua kumpumzisha Eden Hazard na nafasi yake kuchukuliwa na Pedro Rodriguez, mabadiliko hayo yalimsononesha kila shabiki wa Chelsea wakilaumu kwanini aliamua kumtoa Hazard ambaye ni mchezaji anayewapa tabu walinzi wa klabu pinzani kutokana na madhara yake kila anapopata mpira.

Lakini kocha Antonio Conte alijibu mashtaka hayo alipoulizwa kwanini aliamua kumtoa mchezaji huyo, kocha huyo alijibu akisema "Yalikuwa ni mabadiliko ya kimchezo. Inatakiwa uufanye mchezo ulingane kwa dakika zote za mchezo, kama tusingefanya vile basi mchezo usingekuwa sawa."

"Kila mchezaji anajitahidi kucheza soka safi na kuhakikisha timu inakuwa na uwiano mzuri. Narudia tena, sisi kama timu inatakiwa tutafute uwiano wa timu kwenye safu zote za ushambuliaji na ulinzi. Kama ukiwaza kushambulia tu na sio kukaba basi unaweza kupoteza kila mchezo"

Alipoulizwa kama Hazard alikuwa hatimizi majukumu yake na kucheza soka safi ndio maana alitolewa, kocha huyo alijibu akisema, "Hapana, alikuwa ameshaishiwa nguvu, alishachoka"

"Katika kipindi cha kwanza alikimbia sana, na kipindi cha pili alijaribu kufanya ivyo, ila mimi kama kocha, nikimuona mchezaji ameshachoka, ni majukumu yangu kumpumzisha kwa kumfanyia mabadiliko, na ndio maana Pedro aliingia" alisema kocha huyo.

Je una lipi la kuongeza juu ya mtazamo wa kocha Antonio Conte? je alikuwa sawa kufanya mabadiliko ya Hazard?

No comments:

Post a Comment