NYOTA WA CHELSEA KUIKOSA BARCELONA - Darajani 1905

NYOTA WA CHELSEA KUIKOSA BARCELONA

Share This

Mwisho wa wiki hii Chelsea itakuwa nyumbani kucheza mchezo wake wa 30 kwa msimu huu dhidi ya Crystal Palace ambapo mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge. Kuelekea kwenye mchezo huo kuna taarifa mpya zimetoka juu ya nyota wa Chelsea ambaye ni raia wa Brazil, David Luiz kuwa ataendelea kuwa nje zaidi na kuukosa mchezo huo.

Nyota huyo ameanza kwenye michezo mitatu tu toka mwezi Novemba mwaka jana kutokana na majeraha aliyoyapata mwaka 2016, alipochezewa vibaya na nyota wa Manchester city, Sergio Aguero na toka kipindi iko amekuwa akicheza na majeruhi.

Nyota huyo ataikosa michezo mingine ya mwezi Marchi ambapo Chelsea itarudiana dhidi ya Barcelona katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya, lakini pia ataukosa mchezo wa kombe la FA ambapo Chelsea itacheza dhidi ya Leicester city na mchezo wa ligi kuu ambapo Chelsea itamenyana dhidi ya Tottenham.

No comments:

Post a Comment