Kupitia mtandao wa Twitter, moja ya waandishi wa habari alituma ujumbe akiripoti kuwa kocha wa Chelsea, Antonio Conte amefunga mabegi yake na kuachana na Chelsea mara baada ya bodi ya Chelsea kuamua kuachana na kocha huyo mara baada ya kuwa na msimu mbaya huku akitoka kuiongoza vyema mpaka kushinda taji la ligi kuu Uingereza msimu uliopita.
Mwandishi huyo alidai kuwa kocha Antonio Conte ameondoka Chelsea kabla ya baadae fununu hizo kupingwa na mwandishi wa gazeti la Mirror ambae alikuja na kumjibu mwandishi mwenzake ambapo alisema hizo taarifa sio za kweli na kocha huyo bado yupo Chelsea na anaendelea na majukumu yake.
Kocha Antonio Conte ameshindwa kuifanya Chelsea kufanya vizuri msimu huu akishindwa kuiongoza kufanya vizuri kwenye michuano minne ambayo Chelsea imeshiriki msimu huu huku ikiwa na nafasi finyu ya kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao ambapo kwa sasa inashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu Uingereza.
No comments:
Post a Comment