Kuna msemo mmoja wa wazungu unasema ukipiga risasi moja angani basi inaweza ikakosa kumdondosha ndege ata mmoja kati ya makundi mengi ya ndege yanayopita angani lakini kama ukizipiga risasi nyingi hewani unaweza ukabahatisha ukampata ndege ata mmoja. Na hicho ndicho kinachofanywa na Chelsea kwa sasa juu ya nafasi ya kocha Antonio Conte kwenye klabu ya Chelsea.
Chelsea imekataa kupiga risasi nyingi angani ikikataa huenda hiyo risasi moja ikashindwa kumwangushia ndege yoyote na badala yake imeamua kupiga risasi nyingi ambazo huenda mojawapo ikafanikiwa kumwangusha ata mmoja.Chelsea imehusishwa kuwataka makocha wengi ingawa itakubaliana na kocha mmoja tu ndiye atapata nafasi ya kutua klabuni hapo ili kuchukua nafasi ya kocha Antonio Conte.
Lakini kati ya makocha wengi inayohusishwa nayo, kocha mmoja raia wa Italia, Massimiliano Allegri ametoa taarifa mbili zinazokinzana ambapo magazeti mawili ya nchini kwao yameyaripoti ingawa yanatatiza.
Gazeti la kwanza limeripoti kuwa Chelsea imeanza kufanya mawasiliano na kocha huyo aliyewai kukiri kutamani kufanya kazi nje ya Italia ambapo ndipo anapofanya kazi kwa sasa akiwa na klabu ya Juventus huku taarifa hizo zinadai kocha huyo atatua Chelsea endapo atapewa mshahara wa paundi milioni 12 kwa mwaka tofauti na kocha Antonio Conte ambaye analipwa paundi milioni 9. Lakini pia gazeti hilo linakuwa na mashaka mara baada ya kudai kocha huyo ili atue Chelsea basi atatua na wachezaji wake watatu kutoka Juventus ambao ni Federico Bernardeschi, Miralem Pjanic na Rodrigo Bentancur. Lakini mashaka ya gazeti hilo yanakuja wapi? Mashaka ya gazeti hilo yanakuja pale inapoelezwa thamani ya hao wachezaji wengine bado haijajulikana lakini kwa Pjanic dau lake linatajwa kuanzia euro milioni 70, dau ambalo kwa Chelsea ni kubwa kwao kwa mchezaji mwenye miaka 28 au zaidi ya hapo.
Lakini pia wakati gazeti hilo likiripoti hivyo, gazeti jengine limetoa taarifa likidai Chelsea ikishindwa kufudhu kucheza michuano ya klabu bingwa Ulaya kwa msimu ujao basi haitokua na nafasi ya kumnasa kocha huyo.
Lipi ni lipi, jibu kamili litapatikana mwishoni mwa msimu kama kocha Antonio Conte ataamua kuachana na Chelsea na Massimiliano Allegri akaichukua nafasi yake kwa mara ya pili kama alivyoichukua nafasi yake huko Juventus au Chelsea itamnasa kocha tofauti na huyu.
No comments:
Post a Comment