Chelsea inacheza dhidi ya West Ham united mwisho wa wiki hii, ambapo mchezo huo utachezwa siku ya jumapili katika raundi ya 32 ya michuano ya ligi kuu Uingereza ambapo mchezo huo utachezwa pale darajani, Stamford Bridge kwenye jiji la London.
Kuelekea kwenye mchezo huo, Chelsea inaonekana kuwa imara mara baada ya nyota wake wengi kurejea kikosini wakitokea kwenye majeraha.
Thibaut Courtois
Huenda akatumika kwenye mchezo huo ambao Chelsea inahitaji ushindi ili ijiweke sawa katika mbio zake za kutaka kujiweka sawa kwenye mbio za kugombania nafasi ya kucheza michuano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa msimu ujao. Amekuwa majeraha aliyoyapata akiwa mazoezini akijiandaa na mchezo dhidi ya Manchester city.
Lakini sasa anaonekana kuimarika na kuna uwezekano akarejea katika mchezo wa jumapili hii mara baada ya kufanya mazoezi na kikosi cha kwanza.
Pedro
Aliukosa mchezo uliopita dhidi ya Tottenham huku sababu ikiwa majeraha lakini kurejea kwake mazoezini kunaamsha matumaini ya kuweza kutumika kwenye mchezo dhidi ya West Ham.
Ross Barkley
Kucheza kwake kwenye mchezo wa timu ya vijana ya Chelsea ambayo ilicheza dhidi ya Derby County na kurejea kwake mazoezini akiungana na wenzake kunaweza kukamfanya nyota huyo kurejea uwanjani huku mwenyewe akiwa na uchu wa kutaka kufanikiwa ili kujiweka sawa.
No comments:
Post a Comment