Chelsea inashuka kwenye mchezo wa leo wa fainali ya kombe la FA ambapo watacheza dhidi ya Manchester united, mchezo ambao timu mojawapo itaondoka na taji lake pekee kwa msimu huu lakini pia timu nyengine ikibaki bila taji lolote kwa msimu huu.
Kocha wa Chelsea, Antonio Conte hana rekodi nzuri kwenye michezo ya fainali ya makombe kama hizi ambapo hajawai kushinda taji lolote la kombe na leo anacheza dhidi ya timu ya Manchester united iliyoshinda taji hili miaka miwili iliyopita.
Kuelekea kwenye fainali hiyo, hapa nakuletea habari muhimu kuhusu mchezo huo.
Habari muhimu;
Chelsea FC; Emerson Palmieri ataikosa fainali ya leo akiwa sambamba na nyota wenzake, David Luiz na Ethan Ampadu ambao wamekosa michezo mingi wakati Chelsea ilipokua uwanjani.
Chelsea FC inatafuta ushindi kwenye mchezo wa leo ili kuendana na dada zao wa Chelsea Ladies walioshida taji hilo wiki iliyopita wakicheza dhidi ya Arsenal na kuitandika 3-1 kwenye uwanja huuhuu wa Wembley.
Man utd; Romelu Lukaku anaweza akakosekana kwenye mchezo wa leo ingawa hakuna uhakika kama atakuwepo au laah. Kwa upande mwengine kikosi kipo sawia.
Mwamuzi; Michael Oliver ndiye mwamuzi wa mchezo wa leo ambapo mpaka sasa amekua mwamuzi kwenye michezo 36 kwa msimu huu huku akitoa kadi za njano 126 na kadi nyekundu 7.
Rekodi; Mara ya mwisho katika fainali ya kombe hilo la FA ilichezwa mwaka 2007 ambapo Chelsea ilishinda fainali hiyo kwa goli la pekee la Didier Drogba.
Michezo iliyopita;
Chelsea: WWWDL
Man utd: WWLDW
Muda; Saa 07:15 Usiku (Saa 19:15) kwa saa za Afrika Mashariki (EAT)
No comments:
Post a Comment