Kocha wa kikosi cha timu ya soka ya wanawake maarufu kama Chelsea Ladies, Emma Hayes amefanikiwa kujifungua mtoto wa kiume.
Kocha huyo ambaye alishindwa kuongozana na klabu yake hiyo kucheza mchezo wa ligi kuu ambao Chelsea Ladies walicheza dhidi ya Bristol city na kuondoka na ushindi wa mabao 0-2 uliowatangaza kuwa mabingwa wa ligi hiyo maarufu kama FA WSL kutokana na hali yake ya ujauzito kufikia hatua za kujifungua aliiongoza klabu yake hiyo kushinda taji la kombe la FA ambapo Chelsea iliibamiza Arsenal Ladies kwa mabao 3-1 na kulitwaa taji hilo huku akiiongoza pia kwenye michezo ya nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya ambapo Chelsea Ladies ilishindwa kuvuka mbele ya Wolfburg.
Wakati aliposhindwa kusafiri na timu na kujiunga na klabu yake iliposafiri kumenyana na Bristol city, kocha huyo aliutazama mchezo huo kupitia televisheni na wachezaji walisema kocha huyo ni sehemu ya ubingwa huo na hivyo kumshirikisha kocha huyo kabla ya kukabidhiwa kombe la ligi kuu.
Kocha huyo alitangaza kuwa ana ujauzito wa mapacha lakini kwa hali ya kusikitisha pacha mmoja alifariki na sasa ni mama mpya wa mtoto mmoja.
Hongera kwa kocha wetu mzaliwa wa London...
No comments:
Post a Comment