Rasmi; Chelsea yamnasa nyota kutoka Liverpool - Darajani 1905

Rasmi; Chelsea yamnasa nyota kutoka Liverpool

Share This

Klabu ya soka ya wanawake ya Chelsea maarufu kama Chelsea FC Women wamekamilisha usajili wa mlinzi kutoka klabu ya Liverpool, Sophie Ingle mwenye miaka 26 kwa sasa.

Ingle amekamilisha usajili huo huku akisema hii ni nafasi nzuri kwake maana amesaini kwenye klabu bingwa nchini Uingereza ambapo ni kweli klabu hiyo inayofundishwa na kocha Emma Hayes ndio mabingwa wa ligi kuu wanawake nchini humo (FA WSL) pamoja na kombe la FA.

Lakini pia kama haujui, Ingle aliwai kuichezea Chelsea hapo kabla ambapo alitua mwaka 2012 kabla ya 2013 kuondoka na kutimkia kwenye klabu ya Bristol Academy kwa hiyo hii ni kama kurejea kwake Chelsea FC Women ambayo zamani pindi alipokuwepo ilikuwa ikiitwa Chelsea Ladies.

No comments:

Post a Comment