Nyota wa klabu ya Juventus, Danielle Rugani anatajwa kutaka kujiunga na Chelsea ili apate muda wa kucheza zaidi na sio kusalia kwenye klabu hiyo ya Turin nchini Italia ambayo imekuwa haimmpi muda wa kucheza.
Nyota huyo raia wa Italia anatajwa kutakiwa na Arsenal lakini mwenyewe amechagua kujiunga na Chelsea huku thamani yake ikitajwa kufikia paundi milioni 18 kwa sasa akiwa na miaka 23.
Rugani aliwai kutakiwa na kocha Maurizio Sarri pindi kocha huyo alipokuwa akiinoa Napoli na ukaribu wa nyota huyo anayecheza kama mlinzi unatajwa kuchangizwa na kuwai kufanya kazi pamoja pindi walipokuwa kwenye klabu ya Empoli kabla ya nyota huyo kusajiliwa na Juventus kwa dau la paundi milioni 4.
Wakala wa mlinzi huyo anatajwa kuwa kwenye mazungumzo na moja ya viongozi wa Juventus ili kukamilisha biashara zao wakitegemea kumuuza mlinzi huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwaka 2021.
No comments:
Post a Comment