Chelsea inatajwa kukaribia kukamilisha usajili wake wa kwanza katika kipindi iki cha kiangazi mara baada ya mlinzi kijana anayetajwa kuja kutamba baadae, Ian Maatsen kugoma kusaini mkataba mpya kwenye klabu ya PSV na kubwa analodai ni kutaka kutimkia Chelsea.
Maatsen mwenye miaka 16 kwa sasa analazimisha usajili wake wa kuachana na klabu hiyo ya PSV na anachokitaka ni msimu wa 2018-2019 kuutumia akiwa Chelsea.
Chelsea ilidaiwa kumfukuzia nyota huyo hapo kabla lakini PSV ikaonekana kutotaka kumuuza nyota huyo lakini sasa ni kama inabidi wakubali kupokea paundi 97,000 kama dau la mlinzi huyo anayefananishwa na Nathan Ake. Dau hilo ndilo linalotajwa kama thamani yake.
No comments:
Post a Comment